Conférence Episcopale Nationale  du Congo

UJUMBE[1] WA KAMATI YA  BARAZA KUU LA MAASKOFU WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO (JKK) KWA WAKRISTU WAKATOLIKI NA KWA WATU WA MAPENZI MEMA

NIMEIONA TAABU YA TAIFA LANGU (Kut. 3,7)

MNO NI MNO !

 

     Wandugu wapenzi,

1.   Katika mkusanyo wetu uliofanyika pa Kinshasa tarehe 10 mpaka 15 febrario 2003, sisi Maakina, Kardinali, Arkiaskofu na Askofu wanamemba wa Kamati ya Baraza Kuu la Maaskofu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tukiyafanya yetu maneno yake Bwana : “ Nimeiona, nimeiona taabu ya taifa langu” (Kut. 3,7), tunatoa kwa wakristu katoliki na watu wote wa mapenzi mema ujumbe huu :

2.   Kufwatana na kazi ya uchungaji tuliyoamnishwa na katika uaminifu kwa mapokeo ya kinabii katika Eklezia, hatuchoki kulalamika juu ya hali mbaya linamoishi taifa la Kongo. Mbele ya mwanzo wa Mzozo wa wakongomani kati yao, tuliona kama mzozo huo ulikuwa wa lazima sana na hakukua njia ingine[2].  Tuna uchungu mno moyoni kwa kuona ya kwamba Mzozo huu haufikii ukomo wake. Mkataba uliyofanyika pale Sun City haikushikwa, hakuna kitu kilichotendeka na umeongeza tu fujo. Zaidi ya hayo imechongewa vilema vingi mpaka tufikie kwenyi Mkataba mwingine uitwao wa jumla.

 

      Mkataba wa jumla

3.      Wakongomani walipokea Mkataba wa Pretoria III na kitulizo pia na masito. Lakini tangu sahihi iliwekwa juu ya Mkataba huo, wasiwasi la taifa la Kongo imeendelea na kuongezeka pia. Mwisho wa vita unakawia kufika. Mkataba uliofanyiwa na kelele sana ulimwenguni kote hauheshimiwi. Lakini mapambano ya vita yameamka tena katika pande mbalimbali za Kongo na kuleta tena taabu zaidi. Maovu yanatendewa juu ya rahiya na juu ya wafungwa kwa sababu ya vita. Wapiganaji vita wanahepahepa na kuzidisha visingizio ili vita idumu. Mpito hauanzi kamwe. Taabu la rahiya haivumiliki tena.

4.   Kwa kuona hali hiyo isiyoweza kuvumiliwa tena, Sisi, Wachungaji wa taifa la Mungu la hapa Kongo, tunasema : « mno ni mno ! ». Tunawastaki na nguvu yetu yote Washindani kwa ajili ya ujanja wao, kwa ajili ya kutoshtuka kwao   mbele ya taabu ya rahiya, pia kwa ajili ya ukaidi wao wa kufululiza vita.

Ukosefu wa utashi wa siasa na mapendo ya inchi

5.   Ukawio na mambo ya kuzungukana kwa kuheshimu Mkataba wa jumla vinahakikisha ukosefu wa utashi ao moyo wa siasa na mapendo ya inchi dani ya wanaopigana Kongoni. Ngambo zote mbili kuna watu, wachache lakini, wasio na adibisho kamili la siasa wanaoshika taifa nzima kama mateka ; wanatia sahihi juu ya Mikataba, lakini hawafanyi nguvu kwa kuiheshimu. Heshima la ahadi ni fazila wanayozarau.

6.   Kwao, hakuna maambatano kati ya neno na tendo ; hii inashuhudia wazi ukosefu wa ajabu wa roho ao wa utashi ya kuitumikia taifa. Wanafunga na kuvunja bila shida maagano wakifwata tu mapenzi na faida yao peke. Wanasema kitu, lakini wanafanya umbalimbali na yale wanayotoka kusema ; wanaimba amani, lakini wanatumikia vita.

7.   Ukosefu huo wa utashi wa siasa umezaa Mkataba usio na shurtisho wazi la kuacha vita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  upandeni wa waliotia sahihi. Anayesoma Mkataba huo, anashangaa kuona kama hakuna tangazo lolote la kukomesha vita. Lakini Mkataba huo unaonekana kuwa makubaliano tu kati ya wapigana vita, na tuzo kwa wasimamiao vita. Mgawanyo wa uwezo wa kuongoza una na fasi kubwa, kama vile uwezo huo ungalikua ukomo kwa wao wenyewe. Ndiyo sababu mabishano yamefikia kwenyi Mkataba unaoweka fasi ya kwanza wazo la kuchukua uwezo kwa silaha. Lakini rahiya imeishakataa njia hiyo ya silaha[3]. Maana, inaonekana kama haikubaliwe kuendelea kutenda kufwatana na wazo la vita kwani haisaidie kwa maendeleo ya nchi wala kwa kusimika kidemokrasia, ginsi twajuwavyo.   

8.   Watu wa siasa wa nchi yetu hawaonyeshi hata kidogo alama ya mapendo ya nchi. Wakishurulika na faida yao wenyewe, wanafanya siasa kuwa chombo cha pato, hawashuruliki kamwe kutafuta hali nzuri ya rahiya wala kidemokrasia. Vyote ni wazi ; vitendo vya haya walivyotenda huko Sun City,  migawanyo kati yao, shuruli kwa kupata fasi pamoja na magombezi juu ya kuwa mkubwa zaidi ao wa kwanza, hayo yote ni mazoezi yao katika siasa. Watu wa siasa wa kwetu wanashindwa kujisahau na kupigania mbele mafaa makuu ya nchi ; wanafurahiwa tu kutia vikwazo vya kila namna ili vita iendelee katika inchi ya JKK. Hali ya taabu ya rahiya haiwastushe. Hawahangaiki hata kidogo kwa kutafuta kweli kidemokrasia. Tangu hapo, haishangaze tena mtu kuona wanarefusha nyakati za mpito wakizania kama nchi ina feza kwa hayo yote. Tamaa zao za uwezo isiyoriziki imewapeleka kukubali «mpa-ngo wa 1+4 » unaojaa ndani mwake chi-pukizi za ugonvi ku kichwa cha serkali ?.

 

      Uzaifu wa Shirika la kirahiya

9.   Mwanzo wa myaka 90, wakati Shirika la kirahiya ilijipatia matengenezo na kujiunda, wakongomani walifurahi kama wamepata watu wakuweza kutetea na kukinga haki zao. Kuwapo kwa hii shirika la kirahiya katika mambo ya siasa iliamsha kitumaini kikubwa ndani ya watu. Wito wake usio wakisiasa uliiweka Shirika hiyo kuwa chombo cha wanainchi wasiokuwa na tamaa ya siasa ao ya kusharikia nayo. Tumetumainia kama itafanya kazi yake ya muunganisho ; lakini, imejiachilia kuanguka katika fujo. Imegeuka ya kisiasa mpaka ikawa zaifu sana na kuweka katika hatari sifa yake na mafaa za wanainchi.

10. Migawanyo ndani mwake haifaidi kufikia mwisho wa fujo inayotawala inchini. Zaidi ya kupigania uwezo unaowatambulisha wajumbe hawa,  miganyo kati yao na kutumiwa sawa vyombo na wengine hayo yote ni hatari kubwa sana inayopunguza nguvu yao. Ijapokuwa kuna wanaume na wanawake waaminifu, lakini kitendo chao kinasongwa sana na tamaa ya watu wengi wenye kutafuta ukubwa.

 

Juu ya mafaa ya mali na ya siasa, kuna mtu

9.        Mtu, « aliyeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu » (Mw 1, 26), ana bei kupita vitu vyote. Wito wake wa kimtu unamfanya kuwa mtu wa Mungu na mwenye kustahili hesima kubwa sana. Katika JKK, heshima hiyo imezarauliwa kwa ajili ya tamaa ya mali isiyo na mipaka. Vita zinazofwatana katika nchi yetu ni vita tu kwa ajili ya mali. Mali za chini ya udongo ya Kongo imetamaniwa na wenyi nguvu wakitia moto wa magonvi na mgawanyo kati ya wakongomani ili wapate namna ya kuchukua mali hii. Kati ya wanaopata faida katika fujo hiyo wakifichama kuna wanainchi ; wamojawao wametajiwa na ripoti ya ONU. Lakini kuna pia  hasa wageni wanaoiba na ufundi wote mali za Kongo  wao wenyewe ao wakipitia kwa watu wengine. Wanapata faida ndani ya fujo hiyo na wanafanya namna yao yote ili fujo iendelee wapate kushota mali, bila kuishurulikia rahiya iliyo na uwezo juu ya inchi na juu ya mali ya inchi yake.

12. Kwa hawa wote, tunasema kama juu ya mali iliyo chini ya udongo inayotamaniwa  nao sana na yanayowaletea taabu wakongomani, kuna watu ; inafaa kuheshimu ustahili na haki zao. Lalamiko hilo lawaelekea hasa ndugu zetu wanaositasita kwa kujenga amani sababu ya faida yao kuhusu siasa na mali. « Wenyi mali hawadumu » (Zab. 49 [48] 13). Utajiri wa damu haumpe heshima mwenye mali na hauwezi kuwa chemchemu ya raha (cf. Yob. 15, 29). Hivyo hivyo, kutawala kwa ujeuri si kidemokrasia.

Hakuna kutetea mabadiriko ya mipaka ya JKK

11.  Hali ya siasa katika JKK inaonekana kuwa kitisho ao hatari ili nchi yenyewe isiwepo tena. Mbele ya shuruli zote za kugawanya nchi vipandevipande, rahiya ya JKK inakataa mambo haya kwa nguvu yake yote na kupigania umoja wa inchi. Kwa jina la rahiya hiyo, tunaendelea kuhakikisha kwa nguvu yetu yote kama umoja wa nchi na uhuru wa taifa havikubali muteteo wowote[4].  

     Ila tu njia ya amani inaweza kuokoa JKK

14. Njia ya amani peke yake inaweza kutosha Kongo katika fujo, na taifa katika mateso na taabu. Ginsi alivyonena Baba Mtakatifu Papa Yoano Paulo wa II wakati wa kusherehe siku ya amani ulimwenguni kote kwa mwaka wa 2003 na ya ukumbusho wa myaka 4O wa barua “Amani duniani“ (Pacem in terris) ya Mwenyiheri Papa Yoano wa XXIII, hiyo amani -inayotamaniwa sana katika nchi yetu-  ina nguzo nne: ukweli, uhaki, mapendo na uhuru[5]. Wapigana vita na wafanya siasa wanapaswa kujishurtisha kuimarisha nguzo hii nne kwa kuitosha inchi yetu katika hali mbovu. “Kutamani amani si alama ya uzaifu, bali ya nguvu“[6].

15. Kuchagua amani kwashurtisha vitendo vya kuonekana. Hivyo, zaidi ya hotuba na matakio mema, ni lazima wapigana vita na wafanya siasa waonyeshe vitendo vya amani wakiepuka ugonvi unaoleta bure vikwazo katika njia ya kufikia amani. Taifa letu lingefurahi kama wapigana vita wangeweza kutenda vitendo kamili vya amani, kwa mfano kuacha kabisa mapambano, kufanya ibada ya upatanyisho na huruma, mzozo katika ukweli, kuruhusu watu watembee huru na vitu vipite popote katika nchi ya JKK, kuvunja silaha ndogodogo mbele ya watu, na kazalika.

16. Katika hali ya leo ya inchi yetu, njia ya amani yapita hasa kwa heshima ya makubaliano na kutimiza Mkataba uliotiliwa sahihi. Hakika tumeonyesha uzaifu wa Mkataba wa jumla; ijapokuwa hiyo, tuaalika waliotia sahihi juu yake waikamilishe ao waitimize katika yale yanoyoweza kusaidia kuongoza inchi.

17. Hakika, ijapokuwa uzaifu wa Mkataba wa jumla kuhusu mpito katika  JKK, Mkataba huo ni hatua ya lazima katika njia ya kufikia kwenyi amani. Wajumbe katika Mkataba huo wanapashwa waziwazi kukataa vita na ujeuri wowote unaosindikiza vita ; wote waweke silaha chini na kuanza kazi ya kutengeneza jeshi iliyo kama mwanzo wa mpito usiokua na chembe za ugonvi dani.

 

  Mno ni mno !

18. Uzidisho wa vikwazo katika njia ya kupata amani katika JKK umepita kipimo cha uvumilivu wowote. Kufwatana na daraka zetu ndani ya taifa, tunaarifu wapigana vita na wafanya siasa kama: rahiya haitavumilia tena muda mrefu mizungukozunguko yao. Kama fujo inadumu, Kanisa Katoliki litachukua mipango yakufaa  kwa kuharikisha amani katika JKK.

19. Hali ya taabu wanayoishi watu wa Kongo haipashwe kuvunja mgongo wakaaji wa Kongo. Inatuita tujitambue sisi wote kwa kuharikisha ujio wa serekali kamili. Kwa kufikia huko, sisi, Wachungaji na Baba zenu katika imani, tunawaonya na kuwaalika ndugu na dada zetu wapigana vita pamoja na wafanya siasa, waonyeshe utashi wa siasa na alama ya maadibisho ya kweli ya siasa. Waache kupatisha Kongo haya na wageuke viongozi vya kweli wa siasa[7].

20.      Tunawaomba wakristu wenyi kuwa katika Shirika la kirahiya wafanya kweli kazi yao ya kuunganisha watu. Wawe mashuja wanaopigania mema kwa kujenga inchi.

 

Baraka ya mwisho

21. Kwa maombezi ya Bikira Maria Mtakatifu sana, Malkia wa amani, Bwana abariki nchi yetu na amshe dani ya taifa letu wajengaji wengi wa amani.

              Imeandikwa pale Kinshasa, tarehe 15

                                                febrayo 2003



[1] Ujumbe maana yake mu kifransa « message »

[2] CENC, « L’espérance ne déçoit jamais » (Rm 5,5). Le dialogue du peuple congolais, dans la liberté, la justice et la vérité. Message des Evêques de la CENC aux fidèles catholiques et aux hommes de bonne volonté, Kinshasa, Editions du Secrétariat Général de la CENC, 2001, n. 2.

[3] Acte Constitutionnel de la transition, Art. 37.

[4] CENC, « Sois sans crainte » (LC 12, 32). Message des Evêques de la CENC, Editions du Secrétariat Général, Kinshasa, 1999, n. 8.

[5] JEAN PAUL II, Message pour la célébration de la journée mondiale de la paix, Libreria Editrice vaticana, Rome 2003, n. 3.

[6] JEAN PAUL II, « La paix est un devoir pour tous », dans L’Osservatore Romano, n. 31 (31 décembre 2002), p. 3, n. 2.

[7] CEZ, Des dirigeants nouveaux pour le salut du peuple. Message des Evêques du Zaïre aux catholiques et aux hommes de bonne volonté, Editions du Secrétariat Général de la CEZ, Kinshasa, 1995.